Kauli ya Simba baada ya kupangwa tena na Wydad - EDUSPORTSTZ

Latest

Kauli ya Simba baada ya kupangwa tena na Wydad

 Kauli ya Simba baada ya kuangwa tena na Wydad

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Tayari Simba wamewatambua wapinzani wao watakaokutana nao kwenye mechi za kimataifa hatua ya makundi.


Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira imepangwa kundi B ambapo inasaka nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali.


Droo hiyo imechezwa leo Oktoba 6, Afrika Kusini na Simba wameweka wazi kuwa malengo yao ni kupata matokeo kwenye mechi zao za kimataifa.


Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema malengo makubwa ni kutinga hatua ya robo fainali.


“Baada ya kuona wapinzani wetu na timu ambazo tutacheza nao hatuna mashaka ni maandalizi kwa ajili ya mechi hizo ambazo zitafanyika hivi karibuni.


“Tumeliona kundi letu namna lilivyo na tuna wachezaji bora pamoja na benchi la ufundi lenye mbinu hivyo tukutane Robo Fainali,”.


Kundi la Simba lina timu hizi:-Simba, Wydad, Jwaneng Galaxy na Asec Mimosas.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz