Ishu ya jezi feki, Simba na Yanga msikimbilie polisi - Waziri Kijaji - EDUSPORTSTZ

Latest

Ishu ya jezi feki, Simba na Yanga msikimbilie polisi - Waziri Kijaji

 Ally Kamwe.

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Waziri wa Viwanda, Uwekezaji na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji amewataka Wafanyabiashara kuacha kukimbilia Polisi pale wanapopata changamoto ya kibiashara badala yake waende Tume ya Ushindani (FCC).


Dkt. Ashatu ameyasema hayo jana baada ya kutembelea na kukagua ghala lililobainika kuhifadhi jezi bandia za timu za Azam FC, Yanga SC, Simba FC na timu ya Taifa Tanzania.


Waziri huyo amesema Taasisi ya kwanza inayotakiwa kupelekewa malalamiko ni FCC kwa sababu ndiyo yenye mamlaka ya kulinda watumiaji kubaini bidhaa ni bandia au sio bandia, lakini pia kulinda ushindani wenye ufanisi katika biashara.


Aidha, Dkt. Ashatu ametoa siku saba kwa Mkurugenzi wa tume hiyo Wiliam Erio kujiridhisha na kujua idadi halisi ya T-shirt na jezi zote zilipo ili kuhitimisha jambo hili na kushughulika na watu wasioitakia mema Tanzania.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz