Huu ndio muonekano wa Uwanja wa Mkapa - EDUSPORTSTZ

Latest

Huu ndio muonekano wa Uwanja wa Mkapa

 Uwanja wa Benjamin Mkapa

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Kwa kipindi cha miezi mitano Uwanja cha Benjamin Mkapa umekuwa kwenye marekebisho ikiwa ni mpango wa kuufanya kuwa katika hadhi ya viwango vinavyohitajika na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) na hata Shirikisho la Soka Afrika (Caf) ili kuweza kutumika kwenye michezo ya kimataifa.


Ukarabati huo umekuwa na sura mbili ambapo awamu ya kwanza imehusisha maeneo machache ambayo yalitakiwa kutekelezwa kabla ya kuanza mashindano mapya ya African Football League.


Mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo, CAF imepanga ufanyike kwenye uwanja huo ukiikutanisha timu mwenyeji Simba dhidi ya Al Ahly ya Misri, mechi ambayo itapigwa Oktoba 20, 2023.


Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Damas Ndumbaro alitoa tamko kuwa mpaka kufikia tarehe 10 Oktoba uwanja huo utakuwa umemalizika kwa asilimia 100 ya awamu ya kwanza.


Tamko hilo likalisukuma gazeti hili kufunga safari ili kuweza kufahamu nini kinachoendelea kwani 20 Oktoba uwanja huo utafunguliwa rasmi katika uzinduzi wa mashindano mapya kabisa yajulikanayo kama Afrika Ligi yatakayoshirikisha Mataifa manane barani Afrika huku Tanzania ikishiriki Simba SC pekee.


TAA 200 ZA FIFA


Meneja wa uwanja huo Milinde Mahona anasema mpaka sasa katika awamu hiyo ya kwanza ya maboresho wameshaweka taa za kisasa 200 zenye viwango vya CAF ikiwa ni hatua ya kwanza.


Anasema kuwa taa za mwanzo zote zimeondolewa na kuwekwa zenye ubora mkubwa sawa na viwango walivyotakiwa na FIFA kwani ndizo zinazokidhi vigezo vyao vya kuweza kutoa mwanga unaofaa katika mechi kubwa.


“Tunatakiwa kuwa na taa 320 ila kwa kuanzia wametuambia Shirikisho tuanzie na idadi hiyo na uwezo wake ni mkubwa na watu watajionea siku ya uzinduzi kwani mechi itachezwa jioni.”


INTANETI YA KUMWAGA


Meneja huyo amesema watu wote 60,000 ambao uwanja huo una uwezo wa kuwabeba, pamoja na wafanyakazi wa uwanja, kila mmoja atapata huduma ya intaneti.


“Kumekuwa na tatizo la mtandao ndani ya uwanja ndio maana kumewekwa huduma hiyo tena bure na watu wote watakaokuwapo uwanjani hakuna atakayekosa. Intaneti ina nguvu kubwa, ina uwezo wa 10 GB,” alisema.


SHAVU KWA WAANDISHI


Kabla ya marekebisho haya, uwanja huo ulikuwa na nafasi ya waandishi wa habari ambao walikaa jukwaa moja na mashabiki lakini utofauti ulikuwa mmoja tu, viti vya wanahabari vilikuwa na meza.


Sasa meneja huyo anasema marekebisho makubwa yamefanywa kwa upande wa eneo la wanahabari ambapo wamehamishjwa kutoka walipokuwa wakikaa awali na kuhamishiwa eneo la juu zaidi ambalo limejitenga na mashabiki ili waweze kutoa taarifa kwa umma kwa uwepesi na usalama mkubwa.


“Tunaendelea kuboresha eneo lao kwani tumehamisha eneo hilo na kulifanya liwe peke yake ili wasichangamane na mashabiki pia watakuwa na fursa ya kupata huduma ya Intaneti tofauti na wengine.”


“Eneo jipya lina uwezo wa kuhifadhi watu 120 tu na kila mmoja akapata kiti na meza yake, bila kusahau eneo la mikutano ya makocha na waandishi linaendelea kuwekwa sawa na kuwa la kisasa.”


UBAO WA MUDA


Hapo awali kulikuwapo na malalamiko kadhaa kuhusiana na ubao wa matokeo kutokuonyesha katika mechi kadhaa.


Meneja huyo anasema ubao uliowekwa ni wa kisasa ila ni wa muda mfupi kwani bado marekebisho yanaendelea hivyo hawataweza kuweka wa kudumu mpaka watakapomaliza ukaratabati wa uwanja mzima.


“Katika vitu vilivyofanyiwa marekebisho ya muda mfupi ni pamoja na hili kwani tuna malengo ya kuboresha paa la uwanja.”


UWANJA UMENOGA


Meneja anasema uwanja upo katika hali nzuri na kutokana na kutumika kwa muda mrefu kulipelekea kuwa na mabonde ambapo kulisababisha ardhi kuwa ngumu na mbolea kutokukaa vizuri.


“Maboresho ya uwanja hayaishi na haturidhiki tunaona sasa umekaa sawa na FIFA wameupitisha na tunaamini tutakuwa mfano wa kuigwa hata kwa mataifa mengine.


Hata sasa tunaweza kucheza mechi kwani umekamilika na wataalamu wanaendelea kuutunza zaidi,” anasema meneja.


MABANGO YA UMEME


Hapo awali kulikuwa na mabango ya matangazo yaliyozunguka pembeni ya uwanja huo lakini sasa yameondolewa na kuwekwa yale ya kisasa yanayotumia umeme kama ya pale Azam Complex, Chamazi ambayo yameufanya uwanja huo kupendeza zaidi.


Bodi za mabango hayo zilizotengenezwa na kampuni ya Kitanzania zinapatikana katika viwanja vichache Afrika kwani ni za kisasa sana na gharama zake ni kubwa.


Steven Kwezi, Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Formular 360, iliyopewa kandarasi hiyo anasema waliagiza mashine hizo kutokea China kwani hazipatikani hapa nchini.


Anasema kuwa vifaa hivyo vinaweza kukaa zaidi ya miaka sita mpaka 10 vinaweza kuzuia umeme mkali na hata unapokatika ghafla vinaweza kujizima kwa haraka na hata zinapokuwa na shida ni rahisi kujua.


“Hadi kufika Tanzania zimetumia zaidi ya pesa takribani Sh2 bilioni na zinaweza kustahimili mvua kwa kipindi kirefu bila kuharibika,” anasema mhandisi huyo.


“Mabango yanaonyesha matangazo kwa ubora wa hali ya juu na wakati wa mechi wanahitajika wasimamizi wasiopungua watatu kuhakikisha kila kitu cha mitambo hiyo kiko sawa wakati mchezo ukiendelea.


Meneja Mahona anasema vifaa hivyo ni mali halali lakini hawezi kutoa data ambazo sio kamili ila kama mhandisi amesema basi kuna uwezekano kuwa ni kweli kwani wao ndio waatalamu.


“Gharama yake ni kubwa kweli na hii ni moja kati ya maboresho ya muda mrefu tuliyoyafanya katika marekebisho haya ya hatua ya awali kwani vitakaa muda mrefu zaidi.”


VYUMBA VINAWAKA


Marekebisho makubwa yamefanywa katika vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji na yamebaki mambo machache ila kwa upande wa vyoo na mengine yanaelekea kumalizika.


Meneja huyo anasema wamebakiza kuweka vitanda vya kuwanyooshea wachezaji watakapopata changamoto za misuli, televisheni, ubao kwaajili ya kocha kuchorea mifumo au anapoongea wa wachezaji na henga za kutundikia jezi zao wanapojiandaa kuingia uwanjani.


“Wachezaji wetu watafurahia kuwa na sehemu nzuri ya namna hii kwani wakiwa vyumbani wanaweza kujua nini kinaendelea uwanjani lakini pia wanaweza hata kuoga wanapotoka katika mechi,” anasema huku akiwaita mashabiki wajae Oktoba 20.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz