Breaking: Mwakinyo afungiwa kujihusisha na ngumi - EDUSPORTSTZ

Latest

Breaking: Mwakinyo afungiwa kujihusisha na ngumi

 Hassan Mwakinyo.

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) imemfungia Bondia Hassan Mwakinyo kujihusisha na mchezo wa ngumi nje na ndani ya Tanzania kwa muda wa mwaka mmoja na faini ya Tsh milioni 1.


Hatua hiyo imekuja kutokana na kugomea pambano lake lililokuwa lifanyike Septemba 29, 2023, Dar es Salaam dhidi ya mpinzani wake Julius Indongo kutoka nchini Namibia.


Siku moja kabla ya maamuzi hayo kutolewa, kupitia mitandao binafsi ya kijamii ya Hassan Mwakinyo aliandika maneno yafuatayo:


"Nilielewa mapema sana huu mchezo mchafu, nia ovu pamoja na dhamira zenu na hatma iliyotengenezwa kwa thamani ya pesa, nafikiri sasa bila kupepesa macho tunalazimika kuweka vitu wazi wazi hadharani kwenye hili.


"Ili inapotokea tena ishu kama hii kuwe na adabu ya maamuzi hususani kwenye mchezo wetu, ni kweli pesa inaweza nunua haki na utu wa mtu lakini hio ni kwa mtu 'boya' asiyejuwa thamani na haki zake za msingi... see you soon..."Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz