Alichokisema Ally Kamwe baada ya kupangwa na Vigogo hatua ya Makundi CAF CL - EDUSPORTSTZ

Latest

Alichokisema Ally Kamwe baada ya kupangwa na Vigogo hatua ya Makundi CAF CL

 Yanga: Tunakwenda kujipima Makundi CAFCL

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Baada ya Yanga kupangwa kundi “D” ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) ikiwa na Al Ahly, Belouizdad na Medeama Afisa Habari Yanga, Ally Kamwe ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram ya kwamba.


"Kundi D hakuna ubishi, hili ni Kundi Dume kweli, yupo Bingwa mtetezi, Al Ahly, yuko Belouizdad kutoka Algeria, yuko pia Medeama kutoka Ghana.


"Nini msimamo wetu kama Yanga sc? Hii ni nafasi nzuri kwetu kwenda kuipima project yetu ya michuano ya Kimataifa.


"Ni nafasi nzuri kwetu kuipima quality ya kikosi chetu dhidi ya Timu zenye Quality kubwa. Ni nafasi nzuri sana kwetu Yanga kwenda kuitangaza vyema Klabu yetu kwenye michuano ya Kimataifa.


"Siri yetu ya mafanikio ni ileile, kuungana na kushikamana kwa pamoja kama Taasisi. Kila mtu akicheza vyema kwenye Nafasi yake, INAWEZEKANA Daima Mbele Nyuma Mwiko," ameandika Ally Kamwe.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz