Aish Manula kuwavaa Al Ahly?? Hii hapa taarifa Rasmi - EDUSPORTSTZ

Latest

Aish Manula kuwavaa Al Ahly?? Hii hapa taarifa Rasmi


 Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


Baada ya kuwa nje kwa takribani miezi mitano akiuguza majeraha, mlinda lango namba moja wa Simba Aishi Manula yuko tayari kuanza majukumu kwenye kikosi cha kwanza


Jana Simba ilirejea mazoezini Mo Simba Arena baada ya mapumziko ya siku chache Manula akiwa miongoni mwa wachezaji walioshiriki mazoezi hayo kikamilifu


Tanzania One amekamilisha program zote za mazoezi binafsi na sasa amejumuishwa kwenye mazoezi ya timu


Kama Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira ataridhishwa na utimamu wake wa mwili, anaweza kumtumia katika mchezo wa AFL dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Ijumaa ijayo katika uwanja wa Benjamin Mkapa


Ni wazi sasa mchezaji pekee ambaye bado ataendelea kukosekana ni Aubin Kramo kwani hata Hennock Inonga amepona na yuko kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya DR CongoDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz