Ahmed Ally awalipua wanaosema kuwa Simba inapendelewa na waamuzi - EDUSPORTSTZ

Latest

Ahmed Ally awalipua wanaosema kuwa Simba inapendelewa na waamuzi

 Ahmed Ally.

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amewataka wapinzani wao wanaolalamikia kuhusu waamuzi wa Ligi Kuu ya NBC, wapeleke malalamiko yao kwenye vilabu vyao.


Ahmed amesema hayo mara baada ya kujitokeza malalamiko kuwa waaamuzi wanaipendelea Simba na kuipa mabao ya offside.


"Mimi niseme tu kwamba wale wote ambao wana malalamiko na magoli yetu ama na mechi zetu waende kwenye vilabu vyao waweke sanduku la maoni wapeleke malalamiko yao hapo.


"Simba SC wakati tunacheza mechi ya kwanza tunamfunga Mtibwa Sugar bao 4 - 2 hakukuwa na hayo malalamiko, wakati tunakwenda kumfunga Dodoma Jiji goli 2 - 0 hakukuwa na hayo malalamiko, wakati tunakwenda kumfunga Coastal Union bao 3 - 0 hakukuwa na haya malalamiko.


"Wakati wao wanashinda goli tano tano wanawafunga wale vibonde hakukuwa na malalamiko na waamuzi ni hawa hawa, sasa shilingi imegeuka mnyama anaanza kupeleka dozi kwa watu baada ya kuwafunga Tanzania Prisons mabao matatu wengi wakashtuka wakaona Mnyama amedhamiria ubaya baada ya Ihefu kumla mtu wake wa siku zote.


"Wamebadilisha sauti wanasema waamuzi, sisi tunasema kwamba wenye malalamiko apeleke TFF. Sisi tunashinda mechi zetu hatuna kelele na mtu, na kama wana waamuzi wao wawalete tutacheza nao hao hao," Ahmed Ally.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz