Yanga kuvaana na Namungo fc kesho kutwa NBC premier league - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga kuvaana na Namungo fc kesho kutwa NBC premier league

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Al Merrikh katika mchezo wa ligi ya mabingwa uliopigwa Rwanda, kikosi cha Yanga kinarejea katika mikiki mikiki ya ligi kuu ambapo siku ya Jumatano Septemba 20 Yanga inakabiliwa na mchezo dhidi ya Namungo Fc


Mchezo huo wa mzunguuko wa tatu, utapigwa uwanja wa Azam Complex, saa 1 usiku


Itakuwa nafasi nzuri kwa Yanga kurejea juu katika msimamo wa ligi kama wataibuka na ushindi katika mchezo huo


Mashujaa Fc wako kileleni kwa muda baada ya kufikisha alama saba wakishinda mechi mbili na kutoka sare mechi moja


Aidha utakuwa mchezo wa kwanza kwa kocha msaidizi wa zamani wa Yanga Cedrick Kaze kukabiliana na waajiri wake hao wa zamani


Kaze ndiye mkufunzi wa Namungo ambapo mpaka sasa timu yake imeambulia alama moja kutoka mechi mbili walizocheza


Walifungwa na JKT Tanzania katika uwanja wao wa Majaliwa kabla ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na KMC katika uwanja huo huo


KMC na JKT Tanzania zote zilichapwa mabao 5-0 na Yanga katika mechi zao zilizofuata


Ni wazi utakuwa mchezo mgumu lakini malengo ya Kocha Miguel Gamondi na benchi lake la ufundi ni kuona Wananchi wanaondoka na alama zote tatu ili kurejea kileleni mwa msimamo wa ligiDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz