Tambo za Ally kamwe kuelekea mechi ya Yanga vs Al Merrikh ligi ya mabingwa - EDUSPORTSTZ

Latest

Tambo za Ally kamwe kuelekea mechi ya Yanga vs Al Merrikh ligi ya mabingwa


 Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe ametamba kuwa Septemba 30 ni siku maalum kwa Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo kuweka rekodi katika uwanja wa Azam Complex


Ni katika mchezo wa mkondo wa pili kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Al Merrikh


Kamwe amesema msimu huu Yanga iliweka malengo ya kucheza hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa na wamebakisha dakika 90 kuhakikisha wanakamilisha malengo


Kamwe ametamba kuwa Azam Complex utaweka rekodi mpya ya kuingiza mashabiki wengi katika siku hiyo ambayo wataifanya kuwa maalum kwa Wananchi


"Tuliweka wazi mapema, Lengo letu namba moja Wananchi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Msimu huu ni kucheza hatua ya Makundi"


"Mpaka sasa kwa asimilia 50 lengo letu linaelekea kutimia. Tuna Faida mkononi mwetu ya magoli 2-0 tuliyoyapata Ugenini. Kazi imebaki nyumbani"


"Klabu namba tatu kwa ubora wa Afrika kumalizana na Al Merrikh na kutimiza lengo letu. Ni Jumamosi ya kishindo kipya cha Wananchi. Jumamosi ambayo Afrika inatakiwa ilishuhudie Jeshi la kijani na njano kikifanya balaa lake"


"Jumamosi ambayo uwanja wa Azam Complex utaandika Rekodi mpya ya kupokea mashabiki wengi zaidi katika Historia yake tangu ulipozinduliwa," alitamba KamweDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz