Taarifa Mpya kutoka Simba - EDUSPORTSTZ

Latest

Taarifa Mpya kutoka Simba

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 
Daktari wa Simba Edwin Kagabo ameeleza kuridhishwa na maendeleo ya mlinda lango Aishi Manula anayetarajiwa kufanyiwa vipimo vya mwisho na pengine akaruhusiwa kujiunga na wenzake katika mazoezi ya timu


Manula amekuwa nje tangu mwishoni mwa mwezi wa tano, baada ya kufanyiwa upasuaji Afrika Kusini, amefanya program maalum za kumuimarisha na sasa yuko tayari kurejea katika majukumu yake


"Alipewa mazoezi tiba na kuyafanya vizuri, ameimarika kwa haraka sana na baada ya vipimo vya mwisho anaweza kujiunga na wenzake," alisema Kagabo


Manula anaweza kuwa sehemu ya kikosi cha Simba katika mchezo wa kwanza wa robo fainali African Super League dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Oktoba 20, mwaka huu Uwanja wa Benjamin Mkapa


Hii ni habari njema kwa Simba ambayo bado unaweza kusema haijapata utulivu eneo la golikipa tangu alipoumia licha ya Ally Salim kuendelea kuimarika na kufanya vizuri pamoja na ujio wa Ayoub LakredDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz