SINGIDA FG yamuongeza mshambuliaji Bora wa ligi ya kenya - EDUSPORTSTZ

Latest

SINGIDA FG yamuongeza mshambuliaji Bora wa ligi ya kenya

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Imeelezwa kabla ya dirisha la usajili kufungwa usiku wa Septemba 01, Singida Fountain Gate ilikamilisha usajili wa mshambuliaji kutoka Polisi ya Kenya Elvis Rupia


Singida FG ilikamilisha usajili huo muda mfupi kabla ya dirisha kufungwa baada ya kufikia makubaliano ya kuachana na aliyekuwa mshambuliaji wao raia wa Ghana, Bright Adjei


Rupia alikuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Kenya msimu uliopita wa 22/23 akiifungia Polisi Kenya mabao 27


Singida FG ambayo hivi karibuni imemtambulisha Ernst Middendorp raia wa Ujerumani kuwa kocha mkuu, inakabiliwa na ukame wa mabao katika safu yao ya ushambuliaji


Walima alizeti hao wamecheza dakika 180 za mechi mbili za ligi kuu pasipo kufunga bao lolote katika uwanja wao wa nyumbani


Aidha timu hiyo iliponea chupuchupu kuondoshwa na JKU ya Zanzibar katika hatua ya awali kombe la Shirikisho wakikubali kichapo cha mabao mawili na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-3 kufuatia ushindi wa mabao 4-1 katika mchezo wa mkondo wa kwanza


Singida FG itachuana na Future Fc katika mchezo wa raundi ya kwanza kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi CAF CCDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz