Rais Samia atoa Mil. 500 Taifa Stars kufuzu AFCON - EDUSPORTSTZ

Latest

Rais Samia atoa Mil. 500 Taifa Stars kufuzu AFCON

 Rais Samia atoa Mil. 500 Taifa Stars kufuzu AFCON

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametekeleza ahadi ya Shilingi milioni 500 aliyotoa kwa Timu ya Taifa Stars ikifuzu kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 nchini Ivory Coast.


Akizungumza na wachezaji na viongozi wa timu hiyo Septemba 7, 2023 nchini Algeria, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu ambaye aliongoza msafara wa timu hiyo, amewapongeza wachezaji na benchi la ufundi kwa kazi kubwa waliyofanya.


"Kwa niaba ya Serikali, Mhe. Rais, Mhe. Waziri pamoja na wadau wote, tumekuja hapa kuongeza hamasa. Kubwa mtakumbuka wakati wa kujiandaa na mechi ya Uganda kule nyumbani Mhe. Rais alitoa ahadi ya kutoa Shilingi milioni 500, timu ikifuzu.


“Nafurahi kuwaambia kwamba hizo fedha sio tu kwamba zitatolewa, zimekwisha letwa Wizarani kwa ajili yenu," alisema Yakubu.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz