Ngome FC yakana kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Simba - EDUSPORTSTZ

Latest

Ngome FC yakana kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Simba


 Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


Klabu ya Ngome Fc kutoka visiwani Zanzibar imekana kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Simba jana


Mapema jana Simba ilitangaza kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ngome Fc na kuibuka na ushindi wa mabao 6-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Mo Simba Arena


Taarifa iliyotolewa na timu hiyo kupitia kurasa za mitandao ya kijamii, iliitaka klabu ya Simba kuthibitisha kama walicheza mechi hiyo au kurekebisha taarifa waliyotoa mapema siku ya Jumamosi


Hata hivyo klabu ya Simba ilisahihisha na kubainisha kuwa ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ngome Fc ya jijini Dar es salaam


Simba iliibuka na ushindi wa mabao 6-0 katika mchezo huo, mabao yakifungwa na Jean Baleke aliyefunga mawili, Shomari Kapombe, Aubin Kramo,, Willy Onana na Shabani Idd Chilunda


Huo ulikuwa mchezo wa mwisho wa kirafiki kwa Simba kabla ya kuelekea Zambia wanakokabiliwa na mchezo wa ligi ya mabingwa kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi dhidi ya Power Dynamos utakaopigwa Septemba 16 huko Zambia

kumbuka mechi hii itakuwa live kweñye app yetu kama bado huna app yetu 👉👉 BOFYA HAPADownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz