Lomalisa afunguka kilichomliza baada ya rafu ya Manyanya - EDUSPORTSTZ

Latest

Lomalisa afunguka kilichomliza baada ya rafu ya Manyanya

 Joyce Lomalisa.

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Beki wa kushoto wa Yanga, Joyce Lomalisa amekiri rafu aliyofanyiwa na Hashimu Manyanya wa Namungo katika mchezo wa raundi ya tatu Ligi Kuu uliomalizika kwa ushindi 1-0 katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Septemba 20 ilimfanya angue kilio.


Beki huyo akizungumza nasi nakusema kwamba alitokwa na machozi baada ya jaribio la kutaka kuendelea na mchezo huo kushindikana kwa kuwa nia yake ilikuwa ni kuipambani timu.


Lomalisa amesema alitaka kuendelea na mchezo ili aisaidie Yanga ambayo ilikuwa inatafuta ushindi na ulipopatikana ulikuwa umemfuta machozi, huku akionyesha kutofurahishwa na alivyochezewa.


“Sikufikiria kama angefanya kitu kama kile, ndio maana nilienda kwa lengo la kuuchukua mpira pekee, lakini baadaye nikaona amekuja vibaya na aliniumiza sana,” amesema Lomalisa ambaye alitolewa akichechemea baada ya kipindi cha pili kuanza na nafasi yake kuchukuliwa na Nickson Kibabage.


“Nilitaka kuendelea na mchezo ingawa nilikuwa nasikia maumivu, lakini baadaye nikashindwa kabisa na kuomba kutoka. Ni kweli nililia unajua mpaka natoka tulikuwa hatujapata bao na mechi ilikuwa ngumu. Niliumia kuona nashindwa kuendelea kuitumikia timu yangu ikiwa inatafuta ushindi muhimu.”Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz