JKT Tanzania warudi Shinyanga - EDUSPORTSTZ

Latest

JKT Tanzania warudi Shinyanga

 Uwanja CCM Shinyanga

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Kikosi cha JKT Tanzania kitaanza rasmi kuutumia Uwanja wa CCM Kambarage ulioko Shinyanga kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar itakayochezwa Septemba 29, mwaka huu, imefahamika.


Mechi hiyo itakuwa ni ya kwanza ya nyumbani kwa JKT Tanzania na inatokana na kukamilika kwa maboresho kama walivyoshauriwa na Bodi ya Ligi.


Mwenyekiti wa timu hiyo, Kapteni Godwin Ekingo, amesema kikosi chao kilitarajiwa kufika Shinyana jana usiku kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya mechi hiyo ya raundi ya tatu.


“Timu imeshatoka Dar itawasili Shinyanga muda wowote, tuliomba hapa kuwa ndiyo Uwanja wetu wa nyumbani,” alisema Ekingo ambaye timu yake ina pointi tatu ilizopata ugenini katika mechi ya kwanza dhidi ya Namungo.


Naye Meneja wa Uwanja wa CCM Kambarage, Lawrence Manotta, alisema Uwanja huo kwa sasa upo tayari kutumika baada ya kukamilisha maboresho ambayo walitakiwa kuyafanya.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz