Wachezaji wa Yanga ambao wamewasili kambini baada ya majukumu ya Timu za Taifa - EDUSPORTSTZ

Latest

Wachezaji wa Yanga ambao wamewasili kambini baada ya majukumu ya Timu za Taifa

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 
Kiungo wa Yanga Khalid Aucho ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa timu za Taifa ambao walirejea mazoezini jana kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kuwania kutinga makundi ya ligi ya mabingwa dhidi ya Al Merrikh


Aucho alitua juzi kutoka Niger ambako aliiongoza Uganda Cranes kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Niger


Ushindi ambao hata hivyo haukuisaidia Uganda kufuzu michuano ya Afcon 2023, Tanzania ikifuzu baada ya kumaliza nafasi ya pili juu ya Uganda katika kundi F


Aucho ni miongoni mwa nyota 11 wa Yanga ambao walikuwa kwenye majukumu ya timu za Taifa


Wachezaji tisa tayari wamerejea kambini huku Stephane Aziz Ki akitarajiwa kuwasili wakati wowote, mlinda lango Djigui Diarra huenda akachelewa


Leo Mali wanacheza na Ivory Coast ukiwa mchezo wa Kimataifa wa kirafiki

Usikose kutazama LIVE mechi ya El Merrikh vs Yanga na Dynamos power vs Simba mechi zote zitakuwa live kweñye app yetu kama bado huna app yetu 👉👉 BOFYA HAPADownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz