Yanga yakamilisha Pre - Season kibabe - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga yakamilisha Pre - Season kibabe

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Ili kupima utayari wa kikosi chake, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi jana aliwapa nyota wake mtihani wa kucheza mechi mbili za kirafiki asubuhi na jioni


Asubuhi Yanga ilicheza na Friends Rangers na jioni ikashuka tena dimbani kuikabili JKU


Kilikuwa kipimo cha mwisho kwa kikosi kabla ya kuelekea mkoani Tanga kushiriki Ngao ya Jamii


Katika wiki tatu za pre-season, Yanga imecheza michezo minne ya kirafiki ikishinda mitatu na kutoka sare mchezo mmoja


Walianza kwa kuichapa Kaizer Chiefs bao 1-0, wakaichapa Magereza Dar mabao 10-0 jana asubuhi wakaichapa Friends Rangers mabao 6-1 na jioni kutoka suluhu ya bila kufungana dhidi ya JKU


Katika mechi hizo Yanga imefunga mabao 17 huku ukuta wake ukiruhusu bao moja. Wapo ambao watasema baadhi ya mechi zilikuwa nyepesi lakini ni aina ya mechi ambazo zimemsaidia Gamondi kubaini ni kiasi gani wachezaji wake wanaweza kutengeneza nafasi na kuzitumia


Kimbinu, Gamondi hatofautiani sana na kocha aliyepita Nasreddine Nabi, kilichoongezeka kwa Gamondi ni kuwa timu yake inacheza kwa kasi zaidi


Gamondi haruhusu mchezaji kukaa na mpira muda mrefu, ukipigiwa pasi unaachia kisha unawahi kwenye nafasi


Yanga inajenga mashambulizi kutokea nyuma lakini wakivuka katikati ya uwanja kasi inaongezeka


Wakati mwingine timu inaposhambulia walinzi wa pembeni wanaingia kati eneo la kiungo huku mawinga wakikimbiza pembeni na kupiga krosi


Mashabiki wa Yanga watarajie kushuhudia soka lenye kasi ya aina yake, hakuna shaka msimu huu Yanga itafunga mabao mengi Kumbuka mechi zote za ligi kuu zitaoneshwa live kwenye app yetu Bure hivyo kama bado hujaipakua bofya hapaDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz