Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Juzi Yanga Princess ilitangaza kumuuza mshambuliaji wake ambaye pia huitumikia timu ya taifa ya vijana ya wanawake Tanzania, Clara Cletus Luvanga kujiunga na Dux Logrono ya Hispania
Luvanga alijiunga na timu hiyo inayoshiriki ligi daraja la kwanza la Wanawake Hispania kwa mkataba wa miaka mitatu
Leo Yanga Princess imetangaza kumuuza mshambuliaji Blessing Nkor raia wa Nigeria akijiunga na klabu ya Dogus Gold Asyapor ya Uturuki
Nkor alikuwa mshambuliaji kiongozi katika safu ya ushambuliaji ya Yanga Princess msimu uliopita
Katika kipindi cha miaka miwili, Yanga Princess imeuza wachezaji watatu barani Ulaya. Mchezaji wa kwanza alikuwa Aisha Masaka aliyesajiliwa na BK Hacken ya Sweden
No comments:
Post a Comment