Taarifa Mpya kutoka Yanga Mchana - EDUSPORTSTZ

Latest

Taarifa Mpya kutoka Yanga Mchana

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Klabu ya Yanga imetangaza kuzindua 'Documentary' maalum kuzungumzia mafanikio ya Yanga katika msimu wa 2022/23


Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari Serena Hotel mapema leo, Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema Documentary hiyo inakwenda kuhifadhi kwenye historia mafanikio ya Yanga ya msimu uliopita


"Msimu uliopita utahitimishwa rasmi pale msimu mpya unapoanza, Yanga tumejivunia mafanikio tuliyopata msimu uliopita tukifanikiwa kushinda mataji yote ya ndani na kubwa zaidi ni kucheza fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika"


"Tumeandaa Documentary ili kuhifadhi kumbukumbu hii kwa vizazi vijavyo. Ni Documentary ambayo itaonyesha kwa undani yote yaliyokuwa yakijiri nyuma ya pazia hatua kwa hatua hadi kufikia mafanikio tuliyopata"


"Documentary hii iliyotengenezwa kwa utaalamu mkubwa na yenye hadhi ya kuonyeshwa Sinema inakwenda kuwaonyesha Wanachama na Mashabiki wetu maudhui mengi na makubwa ambayo hauwezi kuyapata sehemu yoyote yaliyoiwezesha Klabu yetu kuwa na msimu wa mafanikio na wa kihistoria," alisema Kamwe


Documentary hiyo itazinduliwa siku ya Jumatatu kwenye ukumbi wa Ukumbi wa Sinema Century Cinemax ambapo Wadau, mashabiki na wanachama wa Yanga wataalikwa kushuhudia uzinduzi wake


Baadae itapatikana kupitia Azam Max App kwa kulipia Tsh 2,500/- kuitazamaDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz