Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Klabu ya Simba jana iliendesha mnada wa 'kibegi' ambapo fedha zilizopatikana zinakwenda kusaidia wodi za Mama na Mtoto kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali ya Zanzibar
Katika mnada huo, jezi ya kwanza kunadiwa iliikuwa ya Rais w Heshima wa Klabu ya Simba, Mohamed Dewji ambayo ilinunuliwa kwa shilingi milioni mbili (2,000,000). Mnunuzi ni Bukara Romario, wauzaji wa vifaa vya michezo
- Usikose kutazama live sherehe za Simba Day na mechi ya kirafiki Bure Download app yetu mapema bofya hapa Sasa Ili usipitwe
Jezi ya Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson ilinunuliwa kwa shilingi milioni 2.5 na Tawi la Simba Makini
Jezi ya Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango ilinunuliwa na Sandaland kwa dau la shilingi milioni tatu (3,000,000)
Jezi ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ikanunuliwa kwa shilingi milioni nne (4,000,000) na ES & Sons
Jezi ya Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi ikanunuliwa kwa shilingi milioni tano (5,000,000)
Jezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ikanunuliwa na Benki ya CRDB kwa shilingi milioni 10 (10,000,000) huku kibegi kikinuliwa kwa Tsh Milioni 2.5 na Saleh Majapa
Katika mnada huo Simba imekusanya takribani Tsh Milioni 29
No comments:
Post a Comment