Power Dynamos watatupa mechi nzuri - Chama - EDUSPORTSTZ

Latest

Power Dynamos watatupa mechi nzuri - Chama

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kiungo fundi wa Simba Clatous Chama amesema mabingwa wa Zambia, Power Dynamos watawapa mechi nzuri katika Simba Day Jumapili, August 06 katika uwanja wa Benjamin Mkapa


Chama aliyewahi kuitumikia Power Dynamos kwa miezi sita kabla ya kusajiliwa na Simba msimu wa 2018/19, amesema Power Dynamos ni moja ya timu bora na zenye historia kubwa nchini Zambia


"Power Dynamos ni timu kubwa sana Zambia, wakati naanza kucheza mpira ligi kuu, msimu wa 2009/10, ndoto yangu kubwa ilikuwa kuichezea Power Dynamos, nashukuru nilicheza kwa muda mfupi kabla ya kusajiliwa na Simba"


"Ni timu nzuri walipotea kwa misimu kadhaa lakini nafurahi kuona wamerejea tena wakishinda ubingwa wa Zambia. Natarajia utakuwa mchezo mzuri kwa timu zote"


"Mimi nawaombea washinde mechi yao ya ligi ya mabingwa ili tukutane nao tena ili tuwapige..," alisema Chama


Simba na Power Dynamos zinaweza kukutana kwenye raundi ya kwanza ya ligi ya mabingwa barani Afrika kama Dynamos watashinda mchezo wa hatua ya awali dhidi ya African Star ya Namibia kwani mshindi wa mchezo huo atakutana na Simba inayoanzia raundi ya kwanza



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz