Matokeo Yanga vs KMC Leo 23 August 2023 NBC Premier League - EDUSPORTSTZ

Latest

Matokeo Yanga vs KMC Leo 23 August 2023 NBC Premier League Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Ligi ndio imeanza sasa! Ushindi mnono pamoja na burudani ndio kitu pekee ambacho Wananchi watarajie kutoka kwa timu yao

Ndio! KMC leo wanakuwa mfano kwa wengine watakaofuata baada ya kubamizwa mabao 5-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex

KMC walijitahidi kuzuia kwenye kipindi cha kwanza, Yanga ikifanikiwa kufunga bao moja kupitia kwa nahodha wa mchezo Dickson Job

Hata hivyo kipindi cha pili wakakutana na Yanga yenye ukatili wa aina yake mbele ya lango na kukubali kubugizwa mabao mengine manne

Stephane Aziz Ki alifunga bao la pili kabla ya Hafiz Konkoni kukaribishwa rasmi kwenye ligi kuu ya NBC akifunga bao la tatu Mudathir akaongeza la nne kabla ya Pacome Zouzoua aliyepewa kitengo cha burudani leo akiweka kambani bao la tano

Ni wazi haitakuwa rahisi kuizuia Yanga hii isitetee taji lake msimu huu

Wananchi wameanza na gia ya juu sana...!


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz