Kauli ya kocha wa Yanga kuelekea mechi ya kesho Jumamosi CAF CHAMPIONS league - EDUSPORTSTZ

Latest

Kauli ya kocha wa Yanga kuelekea mechi ya kesho Jumamosi CAF CHAMPIONS league

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema vijana wake wako tayari kwa mchezo wa mkondo wa pili ligi ya mabingwa barani Afrika hatua ya awali dhidi ya Asas Fc


Kesho Jumamosi August 26, Yanga itashuka uwanja wa Azam Complex katika mchezo ambao Wananchi wanahitaji angalau sare Ili kutinga raundi ya kwanza


Gamondi amesema anafahamu mchezo huo utakuwa tofauti na mchezo wa kwanza lakini wamejipanga kuhakikisha wanashinda na kusonga mbele


"Tuko tayari kwa mchezo wa marudiano dhidi ya Asas Fc. Tunafahamu utakuwa mchezo tofauti, wapinzani wetu watajaribu kutushambulia"


"Tutaingia kwenye mchezo huu pasipo kufikiria matokeo ya mchezo wa kwanza, tutahitaji kufunga mabao ili tusonge mbele," alisema Gamondi


Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Azam Complex


Ushindi au matokeo yoyote ya sare yataihakikishia Yanga kusonga mbele raundi ya kwanzaDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz