Fahamu undani wa kocha Robertinho kumpiga chini Phiri - EDUSPORTSTZ

Latest

Fahamu undani wa kocha Robertinho kumpiga chini Phiri

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Mchambuzi wa Soka Edo Kumwembe amefichua siri iliyoko nyuma ya Sakata la Mchezaji wa Simba Moses Phiri kutopewa nafasi ya kucheza katika klabu hiyo.


Amesema Phiri hana maelewano mazuri na viongozi wa Klabu hiyo tangu alipoanza kudai maslahi yake kutokana na mkataba wake unavyosema kipindi anafanya vizuri.


Alikuja na akawa anafanya vizuri sana, anafunga mabao mengi, akapendwa na mashabiki, basi hapo akaanza kudai maslahi yake kutokana na mkataba wake unavyosema.


Bahati mbaya akapata majeraha ambayo yalimuweka nje, ndipo alipoibuka Jean Baleke akawa anafanya vizuri pia basi hapo viongozi ndipo wakaanza kupenyeza 'Vimemo' kwenda kwa kocha kwamba mpange Baleke achana na Phiri.


Makocha pia wanaokuja hapa licha ya kujifanya ni 'Professional' lakini huwa wanajali sana ugali wao, ada za watoto na kodi ya meza hivyo wanawasikiliza sana hawa viongozi wa hivi vilabu, kwani makocha wenye timu Dunianini wachache ukilinganisha na wasiokuwa na timu.


Hivyo wanamkomoa kutokumpa nafasi ya kucheza, nasikia pia Wakala wake alitaka kuvunja mkataba, ameseam Edo.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz