Beno awatumia salam Simba "Soka sio vita" - EDUSPORTSTZ

Latest

Beno awatumia salam Simba "Soka sio vita"

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Golikipa wa Singida Fountain Gate FC, Beno Kakolanya amewatumia salam waajiri wake wa zamani, Simba SC kuwa kikosi chake kinajifua vilivyo kuelekea mchezao wao wa Ngao ya Jamii utakaopigwa katika Dimba la Mkwakwani Tanga, Alhamisi ijayo, Agosti 10 2023.


Beno ambaye alikuwa Simba kabla ya kujiunga na Singida amesema kuwa amepata mapokezi makubwa ndani ya SIngida BF hivyo ana deni kubwa la kuhakikisha anafanya vyema kuisaidia timu yake hiyo mpya.


Singida FG jana ilicheza mchezo wake wa kirafiki na AS Vita Club ya Vongo na kuibuka na ushindi wa bao 2-1 katika Tamasha la Singida Big Day maalum kwa ajili ya kutambulisha wachezaji wao wapya.


“Mpakja mashabiki wananishangilia vile inaonyesha wana Imani kubwa na mimi na kuna kitu wanakitarajia kutoka kwangu, nimefurahi kwa mapokezi walionipa.


“Kuelekea mechi dhidi ya Simba, niwaombe mashabiki wa Singida wawe na Imani na timu yao, kwa sasa tunaendelea kujifua ili kutengeneza muunganiko kwa sababu wachezaji wengi ni wapya, kwa hiyo mpaka mechi ya Simba itakapofika tutakuwa tumekaa vizuri, mpira sio vita.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz