Alichokisema Maxi NZENGELI baada ya Yanga kuonesha upendo huu kwake - EDUSPORTSTZ

Latest

Alichokisema Maxi NZENGELI baada ya Yanga kuonesha upendo huu kwake

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kiungo mshambuliaji wa Yanga Maxi Mpia Nzengeli amewashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa sapoti kubwa waliowapa wachezaji katika mchezo wa mkondo wa pili ligi ya mabingwa hatua ya awali dhidi ya Asas Fc


Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Azam Complex, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 5-1


Mchezo huo ulikuwa maalum kwa Maxi, mashabiki wakichomokea mavazi yao ikiwa ishara ya kumuunga mkono


"Nawashukuru mashabiki wa Yanga kwa tukio hili walilofanya nafikiri litabaki katika kumbukumbu ya maisha yangu kwa muda mrefu. Nimeona hamasa kubwa kabla ya mchezo na kuendelea siku ya mchezo"


"Katika maisha yangu hii ni mara ya kwanza kukutana na tukio kama hili, hii ni heshima kubwa kwangu"


"Ninachowaomba mashabiki waendelee kutuunga mkono wachezaji wote na matukio haya yaendelee kwa kila mchezaji," alisema Maxi


Naye Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema matukio maalum ya kuwaongezea thamani wachezaji yataendelea kwenye mechi zote za Kimataifa


"Huu ni mwanzo tu, tutaendelea kwa wachezaji wengine wote. Kutakuwa na siku ya Zouzoua na hapa nimepokea meseji nyingi kutoka kwa kinadada wanataka itakayofuata iwe maalum kwa Aziz Ki sijajua wanataka kufanya nini siku hiyo," alibainisha KamweDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz