Alicho kiandika Msemaji wa Simba kwa wale wanaobeza mpira wa Simba wanao cheza - EDUSPORTSTZ

Latest

Alicho kiandika Msemaji wa Simba kwa wale wanaobeza mpira wa Simba wanao cheza

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema wachezaji na benchi la ufundi wanastahili pongezi kwa kucheza mechi nne ndani ya siku 12 na kuweza kushinda zote


Ahmed amesema ni shauku ya Wanasimba kuona timu yao ikicheza soka la kuvutia maarufu 'pira biriyani', lakini jambo muhimu kwanza ni kuhakikisha timu inashinda mechi zake hivyo kocha Robertinho Oliveira ameanza kutengeneza timu ya ushindi kwanza


Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Ahmed ameandika ujumbe huu;


"Wachezaji wetu na Benchi la Ufundi wanastahili pongezi, wamecheza 4 ndani ya siku 12 na zote wamepata ushindi


Kwa interval hiyo usitegemee timu kucheza kwa kiwango kikubwa sana bali ni kucheza kwa malengo


Pamoja na hayo kikosi chetu kina wachezaji wapya 11, ni ngumu mno timu yenye maingizo mapya kucheza kwa maelewano makubwa


Kwa kufahamu hilo Mwalimu Robertinho ameanza kwanza kutengeneza timu ya ushindi baada ya uhakika wa ushindi ndipo atageukia mpira mzuri


Kwenye kuhakikisha timu inapata kwanza ushindi, Mwalimu anatumia zaidi Wachezaji wa zamani huku wale wapya akiwapa nafasi mmoja baada ya mwingine


Wana Lunyasi tuendelee kuwa na imani na Mtaalamu Robertinho na tumpe muda wa kufanya kazi yake


Kutengeneza Pira Biriani inahitaji sana muda


Ukitaka kuamini kucheza pira biriani sio jambo dogo kuna watu hawajawahi kucheza mpira huo tangu kuumbwa kwao" Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz