Yanga yapewa mwaliko na Rais wa Malawi - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga yapewa mwaliko na Rais wa Malawi

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wamealikwa nchini Malawi kwenye maadhimisho ya sherehe za Uhuru wa nchi hiyo ambazo zitafanyika Julai 06 2023


Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema kwa heshima waliyopewa na Malawi, wamelazimika kuwaita wachezaji kambini kwa ajili ya kuhudhuria mwaliko huo wakiongozana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Samia Suluhu Hassan


Kamwe amesema wachezaji 15 wa kikosi cha kwanza wataambatana na wachezaji wengine sita kutoka timu ya vijana


Kamwe amesema mwaliko huo ni matokeo ya mafanikio ambayo Yanga wamepata katika misimu miwili iliyopita


"Tumepokea mwaliko maalumu kutoka kwa Serikali ya Malawi kucheza mchezo maalumu kwenye maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Malawi itakayofanyika Julai 6, 2023. Hii ni heshima ya kipekee kwa Tanzania na klabu ya Yanga kualikwa kwenye sherehe kubwa ya nchi ambayo itawakutanisha marais wa nchi mbalimbali akiwemo Rais wa Tanzania Mama Samia Sluhu Hassan"


"Mwaliko huu unatosha kuonyesha ukubwa wa klabu yetu na heshima ambayo tunapewa huko nje. Kwa mara nyingine tutakwenda Malawi kwa ndege maalum ambayo itaturudisha nchini baada ya mchezo. Kwa wale walioumia tuliposafiri na Ndege maalum kwenda Algeria basi waumie na hii," alitamba Kamwe


Wachezaji wanatarajia kuripoti kambini siku ya kesho Jumanne na timu kuondoka nchini mapema siku ya JumatanoDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz