Yanga wakanusha kuibiwa mchezaji na Simba Airport - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga wakanusha kuibiwa mchezaji na Simba Airport

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Leo  huko kwenye mitandao ya kijamii kumeibuka tetesi kuwa kuna mchezaji amepokwa huko uwanja wa ndege akiwa ametua nchini kwa ajili ya kujiunga na Yanga


Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesisitiza kauli yake aliyoitoa jana kuwa walishafunga usajili wa msimu huu hivyo kinachoendelea ni maigizo tu


"Tulijua haya yatatokea ndio maana tukasema mapema kuwa tumeshafunga usajili, wachezaji wote tuliowahitaji wameshasaini mikataba yao zoezi lililobaki ni kuwatambulisha tu"


"Leo usiku tutatambulisha mchezaji mmoja halafu hao wengine tutawatambulisha kwa utaratibu ambao tumeuandaa"


"Sisi hatununui wachezaji 'online', Wananchi watulie muda wa kushusha vyuma umekaribia," alisema Kamwe


Kiungo Fabrice Ngoma ndiye anayetajwa kutua nchini kujiunga na Simba, kumekuwa na mjadala kuwa ndiye namba sita ambaye Kamwe amekuwa akitamba nae kwa wiki kadhaa


Kamwe amesema Wananchi watulie namba sita wao yupo na watamtambulisha katika wakati mwafakaDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz