Yanga waambulia patupu Usajili wa Chivaviro, atambulishwa Kaizer Chiefs - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga waambulia patupu Usajili wa Chivaviro, atambulishwa Kaizer Chiefs

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini imethibitisha kumsajili mshambuliaji Ranga Chivaviro kutoka klabu ya Marumo Gallants iliyoshuka daraja.


Chivaviro (30) raia wa Afrika Kusini amesaini mkataba wa miaka miwili wenye chaguo la kuongezeka kwa mwaka mmoja zaidi.


Kupitia taarifa yake kwa umma Kaizer Chiefs imeandika:- “Tunapenda kuthibitisha rasmi usajili wa Ranga Piniel Chivaviro kutoka Marumo Gallants. Ametia wino kwenye karatasi baada ya kukubaliana na mkataba wa miaka miwili na chaguo la mwaka mmoja. Atavaa jezi maarufu #7”


Mshambuliaji huyo alikuwa akitajwa kuhitajika na Yanga na sasa ni dhahiri kuwa Yanga wamekosa huduma yake msimu huu.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz