Tutatangaza mshambuliaji kabla ya dirisha kufungwa - Kamwe - EDUSPORTSTZ

Latest

Tutatangaza mshambuliaji kabla ya dirisha kufungwa - Kamwe

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema wako kwenye hatua za mwisho kukamilisha usajili wa mshambuliaji mpya ambaye atakuja kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji


Kamwe amesema ni mapendekezo ya kocha Miguel Gamondi baada ya kukifanyia tathmini kikosi chake


"Ni kweli kabla ya dirisha la usajili kufungwa, tutaleta mshambuliaji mwingine ambaye atakuja kushirikiana na hawa waliopo. Kocha wetu (Gamondi) ameridhika na kila nafasi tuliyofanya maboresho lakini akapendekeza tuongeze nguvu katika eneo la ushambuliaji"


"Tuko kwenye hatua za mwisho kukamilisha usajili wa mshambuliaji huyo ambaye tunaamini ataendeleza burudani kwa Wananchi kwa kufunga mabao," alisema Kamwe


Dirisha la usajili CAF litafungwa Jumatatu, Julai 31 hivyo ni wazi Yanga inapaswa kukamilisha usajili wa mshambuliaji huyo kabla ya Jumatatu


Bado Yanga haijatangaza kumuuza mshambuliaji Fiston Mayele wakisubiri klabu iliyomsajili (Pyramids Fc) ikamilishe mchakato wote wa kumsajiliDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz