Ten Hag kichwa kinawaka moto - EDUSPORTSTZ

Latest

Ten Hag kichwa kinawaka moto

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA.


 Erik ten Hag na chama lake la Manchester United ametua Oslo na maswali kibao kichwani mwake.


Wiki sita zilizopita, chama lake la Man United lilicheza fainali ya Kombe la FA na kuchapwa na mahasimu wao Manchester City uwanjani Wembley.


Man United ilicheza mechi hiyo ikiwa na shida nyingi. Bado haijamaliza shida yake ya kukosa straika wa maana.


Hilo bado halijatatuliwa, Ten Hag bado anakabiliwa na matatizo kibao wakati huu akijaribu kukijenga kikosi chake kuwa na nguvu kubwa kwa ajili ya msimu ujao.


Matamanio ya Ten Hag ni kuendeleza mwanzo wake mzuri kwenye kikosi hicho cha Old Trafford baada ya kufanya vizuri katika msimu wake wa kwanza, ambapo Man United ilimaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England na kukamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu ujao.


Man United ilibeba pia taji lao la kwanza tangu mwaka 2017, iliponyakua Kombe la Ligi baada ya kuichapa Newcastle United kwenye mchezo wa fainali uliofanyika Wembley.


Kulikuwa na mambo mengi chanya pia baada ya kufika fainali ya Kombe la FA. Lakini, kwenye fainali hiyo walionyesha uhalisia wao kwamba bado wapo nyuma sana kiviwango na mahasimu wao Man City baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1, katika mechi ambayo chama la Pep Guardiola lilionekana kutawala kila eneo.


Baada ya fainali hiyo ya Wembley, swali kubwa lililoibuka nini kinafuata kwa Man United?


Na jana Jumatano walipokuwa wakikabiliwa na mechi ya kirafiki dhidi ya Leeds United, Man United haikuwa na chaguo la kwanza golini baada ya kipa wao namba moja, David de Gea kuondoka na bado hawajakamilisha dili la kumnasa kipa mpya, Andre Onana kutoka Inter Milan.


Hawana Namba 9 anayetambulika huku kwa muda mrefu wakihusishwa na Harry Kane, ambaye mapema tu kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi walipata majibu kutoka kwa mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Levy kwamba hayupo tayari kufanya nao biashara.


Jambo hilo limewasukuma kuhamia Serie A kwenda kupambana kunasa saini ya straika wa Denmark mwenye umri wa miaka 20, Rasmus Hojlund, ambaye msimu uliopita alifunga mabao 10 akiitumikia Atalanta.


Naye bado hawajamsajili huku Atalanta ikimthaminisha straika huyo kuwa na thamani ya Pauni 50 milioni, huku Man United ikimwona mshambuliaji huyo hajafikia thamani hiyo.


Wazo la kuanza msimu mpya wa 2023-24 na huduma ya Anthony Martial kwenye safu ya ushambuliaji si kitu kinachowaingia kabisa akilini mashabiki. Shida ya mashabiki wa Man United kwa Martial wanamwona kama mchezaji ambaye haonekani kujali sana mpira. Anacheza kwa kujisikia na wala si majeruhi.


Kuna ishu nyingine pia, inaonekana kama mfungaji wao mahiri kwa sasa Marcus Rashford amesahaulika, wakati alionyesha kiwango bora sana alipofunga mabao 30 katika mechi 56 alizocheza msimu uliopita.


Shida inayomhusu Rashford ni kwamba bado hawajasaini mkataba mpya na anakwenda kuingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake wa sasa. Ten Hag hapendezwi na hilo, ila maswali yatazidi kumwaandamana kwenye mikutano na waandishi wa habari kwanini ishu ya mkataba mpya wa Rashford bado haijakamilishwa.


Mashabiki hawataelewa kama timu itaingia uwanjani msimu ujao ikiwa na huduma ya Martial kwenye fowadi. Mchezaji mwenyewe hana shida, bado anahitaji kubaki Man United, lakini je kuna kitu alichofanya cha maana cha kuendelea kubaki kwenye timu hiyo na kulipwa mshahara unaokaribia Pauni 300,000 kwa wiki?


Kuna ripoti inadai kwamba, Rashford anasubiri kwanza kuona ni wamiliki gani wapya watakuja kuchukua mikoba ya kuimiliki timu hiyo ndipo hapo atakapoamua kusaini dili jipya au la.


Ndiyo, anasubiri mmiliki mpya. Hiyo ni ishu ambayo imekuwa ikijadiliwa tangu Novemba mwaka jana.


Sir Jim Ratcliffe na Sheikh Jassim wanachuana kuimiliki timu hiyo kutoka kwenye mikono ya familia ya Kimarekani ya Glazer. Familia hiyo ya Glazer wanaithaminisha Man United kuwa na thamani ya Pauni 6 bilioni na wanataka ilipwe pesa hiyo ili wafanye biashara, wakati matajiri hao wawili, ofa yao kubwa ni Pauni 5.5 bilioni.


Dili la kuiuza Man United bado halijakamilishwa na pengine hilo linaweza kuchochea jambo la maandamano ya mashabiki na Ten Hag akakutana na mabango mengi katika kila mechi watakacheza Old Trafford msimu ujao.


Mashabiki wa Man United wameandamana na hawataacha kufanya hivyo hadi hapo timu hiyo itakapoouzwa jumla.


Man United imetumia pesa nyingi sana kwenye usajili kwa muongo mmoja uliopita, lakini ndani ya muda huo, imeshuhudia pia Pauni 1 bilioni ikitoweka tu kulipia madeni ya wamiliki wa klabu hiyo, familia ya Glazer na ndio maana mashabiki wanataka timu iuzwe.


Wakati dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi likiwa wazi na kila timu inajaribu kusajili kujiweka sawa, bajeti ya Ten Hag kwenye usajili inatajwa kuwa ni Pauni 120 milioni tu.


Tayari Pauni 55 milioni, ambayo itaongezeka hapo baadaye na kufikia Pauni 60 milioni kutokana na nyongeza nyingine zimeshatumika kwenye usajili wa Mason Mount, ambao ndiyo usajili pekee uliothibitishwa hadi sasa, wakati kiungo huyo mshambuliaji alipotoka Chelsea na kutoka Man United.


Hivyo hawana salio la kutosha kwenye bajeti yao ya usajili na bado hawajapata kipa wa maana na straika wa maana ili kufanya timu kuwa na uwezo wa kushindana msimu ujao. Kuwa na pesa za kusajili kama timu itakuwa haijauzwa, basi Man United itahitaji kuuza wachezaji wake kwanza.


Bahati mbaya kwa Ten Hag hakuna mtu anayekwenda kubisha hodi mlangoni kwake kuhitaji huduma ya mastaa wake, miongoni mwa waliowekwa sokoni ambao ni Martial, Fred, Scott McTominay na nahodha Harry Maguire.


Ni matatizo juu ya matatizo yanayomwandama Ten Hag. Wachezaji wake hawauziki ili apate pesa ya kusajili wapya.


Kuna makosa mengi yalifanywa na watangulizi wake kuanzia David Moyes na Louis van Gaal, huku Jose Mourinho akija kuongeza matatizo zaidi kabla ya kuja Ole Gunnar Solskjaer, aliyekuwa na ndoto nyingi ambazo pia zilishindwa kutokana na kuwapo kwa kundi kubwa la wachezaji waliokuwa na viwango vya kawaida sana kwenye kikosi.


Kama Man United itaendelea kubaki kama ilivyo, basi kila mtu wataendelea kuwashuhudia mahasimu wao Man City wakiendelea tu kujinyakulia mataji na Guardiola kuendelea kuvuta zile sigara zake kuonyesha ubabe.


Ten Hag anajaribu kutengeneza kikosi chake. Aliwaleta Antony na Lisandro Martinez kutoka Ajax mwaka jana, kisha wakaja kuungana na wakali wengine kama Casemiro na Raphael Varane kwenye timu kuifanya kuwa imara kwenye baadhi ya maneo. Kwenye dirisha hili angependa kuwa na huduma ya kipa mpya, straika mpya, beki wa kulia mpya, kiungo wa kukaba mpya na beki wa kati mpya, ili kikosi kiwa na uwezo wa kushindania mataji.


Bahati mbaya hadi sasa, bado hakijaeleweka, huku kikosi hicho kikianza mazoezi ya pre-season kukiwa na mambo kibao yanayoibua maswali ya kutosha na mustakabali wa kikosi hicho kwa msimu ujao.


MATATIZO SABA YANAYOSUMBUA KICHWA CHA TEN HAG MAN UNITED KWENYE KIPINDI HIKI CHA PRE-SEASON


1.Hakuna kipa mpya baada ya De Gea kuondoka


2.Hakuna straika mpya licha ya kumsaka Harry Kane


3.Hakuna anayetaka kununua wachezaji kama Harry Maguire


4.Hakuna mmiliki mpya licha ya mazungumzo ya muda mrefu


5.Hakuna mpango wa mashabiki kuacha kuandamana dhidi ya Glazer


6.Hakuna dili jipya la mshambuliaji Marcus Rashford


7.Hakuna dalili za kuifikia Man City kiubora uwanjani


Chanzo: Mwanaspoti



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz