Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kocha mkuu wa Klabu ya Simba SC, Roberto Oliveira Gonçalves do Carmo 'Robertinho' amezungumzia droo ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika #TotalEnergiesCAFCL ambayo imefanyika jana.
Robertinho amesema ana amini wana timu nzuri na benchi la ufundi lenye ueledi wa hali ya juu na hiyo haiwezi kuwa sababu ya kuwadharau wapinzani wao watakao kutana nao.
Kocha huyo ambaye ametua juzi kambini Uturuki akitokea nyumbani kwao Brazil akaongeza kuwa ukiwaza kikubwa unakuwa mkubwa pia , hivyo Simba imeshatengeneza mazingira hayo ya kucheza kwenye hatua kubwa.
"Kwa sasa tuna timu moja imara, tunajivunia benchi bora la ufundi, wataalam, na wanatoa kipaumbele kwa ushindi na performance kubwa. Ninawaheshimu wapinzani wote wawili, lakini kwangu ninafikiria mbele zaidi. Ukifirikia mbele zaidi unakuwa mkubwa, Simba iko tayari kucheza na timu za kiwango cha juu," amesema Robertihno.
Mwisho akawaomba mashabiki kutoa sapoti kwa wachezaji na timu kwa ujumla kwani anaamini nguvu ya mashabiki ni kubwa sana ndiyo maana ya mchezaji wa 12 na Nguvu moja.
"Mashabiki, ninawaomba muwasapoti wachezaji wetu, muisapoti timu, kwa sababu mkitupa ushirikiano wetu sit u kwamba tutacheza kama wachezaji 11 uwanjani bali wachezaji 12, Simba Nguvu Moja,” amemaliza Robertinho.
Simba Sc haitocheza hatua ya awali lakini katika hatua ya kwanza watacheza na mshindi kati ya Africans Stars ya nchini Namibia au Power Dynamos ya nchini Zambia.
Post a Comment