Mwisho wa hadithi tamu ya Bangala na Djuma ndani ya Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Mwisho wa hadithi tamu ya Bangala na Djuma ndani ya Yanga

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Mwisho wa Djuma Shabani na Yannick Bangala ndani ya Yanga ulianza muda kidogo. Wote wawili hawajaachwa kwa sababu ya kupungua ubora wao uwanjani, sababu kuu ya kuachwa ni hii hapa....


Wanazuoni husema, 'Ngoma ikilia sana ujue inakaribia kupasuka', wa-Congo hao baada ya kupata majina walianza kutanua makwapa mithiri ya mtu aliyebeba ndoo za maji.


wa mujibu wa ripoti ya aliyekuwa kocha wa Yanga SC, Nabi Wachezaji hao walikuwa wakiendesha migomo ya chinichini kambini, that's why alipendekeza waachwe.


Mwishoni mwa 22/23 watu wengi walijiuliza kwa nini Bangala anakaa benchi ? Kwa nini Djuma game time yake imepungua ?


Majibu alikuwa nayo Nabi, aliwaorodhesha miongoni mwa Wachezaji (3) wasio na nidhamu ambao wanatakiwa kuachwa ;


Bernard Morrison


Djuma Shabani


Yannick Bangala


Baada ya kulibaini hilo, Djuma na Bangala walitikisa kiberiti kuelekea mwisho wa msimu 22/23, waliuambia uongozi wa Yanga wanataka kuondoka, ili wabaki wanaomba wapandishiwe mishahara.


Tofauti na mategemeo yao, Uongozi wa Yanga ulikubali ombi lao la kutaka kuondoka.


Ikumbukwe, Yanga ndio klabu pekee Tanzania iliyowahi kutimua Wachezaji wote kikosini kwa hiyo wakaendeleza utamaduni wao wa kusimamia misimamo yao bila kujali ukubwa wa majina ya Bangala & Djuma Shabani.


Jambo hilo liliwashitua Wachezaji hao ikabidi waende kuomba msamaha kwenye uongozi wa Yanga ili warejee kikosini.. Uongozi wa Yanga ukawaambia Too late tayari wameshasajili Wachezaji wengine.


Huo ndio ukawa mwisho wa MVP wa ligi kuu 21/22 Yannick Bangala na mwisho wa Djuma Shabani The most assist defender 21/22 katika klabu ya Yanga



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz