Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Lengo la matamasha hayo ni kutoa misaada mbalimbali na kurudisha kwa Jamii
Tamasha la kwanza litafanyika leo Julai 2, 2023 mkoani Tanga ambalo litahusisha timu ya Mwamnyeto na Mauya dhidi ya timu ya mkoa wa Tanga. Tamasha la pili litafanyika Julai 7, 2023 mkoani Morogoro
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ambaye juzi alikuwa mkoani Morogoro kuwaunga mkono Kibwana Shomari na Dickson Job katika tamasha kama hilo, anatarajiwa kuwa mkoani Tanga kuwaunga mkono Mauya na Mwamnyeto
Matamasha yote mawili yanahusisha mambo mawili, jambo la kwanza ni kutembelea vituo vya watu wenye uhitaji maalum na jambo la pili itakuwa ni mechi ambayo itahusisha timu itakayoundwa na Mwamnyeto na Mauya na watu wao dhidi ya combine ya Mkoa wa Tanga pamoja na Morogoro
Post a Comment