Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Simba ilikuwa ya kwanza kufunga bao la kuongoza kupitia kwa Kibu Denis aliyemalizia pasi murua ya Saido Ntibazonkiza
Bao la Zira Fc inayoshiriki ligi kuu ya Azerbaijan, lilifungwa na Rustam Ahmadzade
Katika mchezo huo Simba ilianza na Ali Salim, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Hennock Inonga, Che Malone, Mzamiru Yassin, Kibu Denis, Sadio Kanoute, Moses Phiri, Saido Ntibazonkiza na Willy Onana
Katika kipindi cha Aubin Kramo aliingia kuchukua nafasi ya Phiri, Clatous Chama akaingia nafasi ya Onana, Bocco akaingia kuchukua nafasi ya Kramo aliyepata majeraha, Fabrice Ngoma akaingia nafasi ya Sadio Kanoute na Isarael Mwenda akaingia nafasi ya Kibu Denis
Huu ni mchezo wa kwanza wa kujipima kwa Simba baada ya wiki mbili za mazoezi huko Uturuki
No comments:
Post a Comment