Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kamwe amesema hayo leo wakati akihojiwa na WASAFI FM kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwenye Siku ya Mwananchi.
"Kesho tuna mambo makubwa matatu, la kwanza ni kuhakikisha mashabiki, wananchama wa Yanga na Watanzania wote watakaokuja Benjamin mkapa watakuja ku enjoy mchezo mzuri wa kaizer Chiefs na Ynaga.
"Uzuri wa Kaizer wamekuja kamili, wamesema hawajaja kutalii, wamekuja kuhakikisha wanapambana na Yanga kupima kikosi chao kwa ajili ya msimu unaokuja. Na sisi itakuwa sehemu sahihi ya kupima wachezaji wetu ambao tumewasajili kwa ajili ya msimu ujao.
"Kutakuwa na mechi ya viongozi wa Yanga na wasanii wa Bongo Fleva na Bongo Movies. Pia, kutakuwa na utambulisho maalum kwa wachezaji wetu tutakaokuwa nao msimu ujao.
"Watu wanauliza nani atatambulisha wachezaji hawa? Hii tuiache kama sapraizi, kesho wataalam waliokabidhiwa kazi hiyo. Mtu ambaye tutampa jukumu la kutambulisha hawa wachezaji ni mwamba kwelikweli, lazima awe fundi kuhakikisha wananchi wana burudika," amesema Kamwe.
No comments:
Post a Comment