CAF yaondoa play-off Shirikisho - EDUSPORTSTZ

Latest

CAF yaondoa play-off Shirikisho

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limefanya mabadiliko katika timu zinazokata tiketi ya kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na kombe la Shirikisho


Katika misimu ya nyuma ilizoeleka timu 16 zilizotolewa raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa zilipewa nafasi ya kucheza mtoano kombe la Shirikisho ili kukata tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya Shirikisho


Kuanzia michuano inayofuata, timu zitakazotolewa raundi ya kwanza ya ligi ya mabingwa zitaondoshwa mashindanoni kwani hakuna tena nafasi ya kupelekwa kucheza Shirikisho


Hivyo timu 16 zitakazofuzu raundi ya pili ya Shirikisho, zitatinga moja kwa moja hatua ya makundi


Kwa maana rahisi ni kuwa timu zitakazocheza ligi ya mabingwa hazitakuwa na nafasi ya kucheza kombe la Shirikisho katika msimu huo


Na zile zinazocheza Shirikisho tangu mwanzo ndizo zitakazokutana katika hatua ya makundi



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz