Alicho kusema kocha wa Yanga kuelekea mechi ya kesho dhidi ya Kaizer Chief - EDUSPORTSTZ

Latest

Alicho kusema kocha wa Yanga kuelekea mechi ya kesho dhidi ya Kaizer Chief

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema vijana wake wako tayari kwa mechi muhimu ya maadhimisho ya wiki ya Mwananchi dhidi ya Kaizer Chiefs


Mchezo huo utapigwa kesho Jumamosi, saa 1 usiku katika uwanja wa Benjamin Mkapa


Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Gamondi amesema ni siku kubwa kwa mashabiki wa Yanga kuukaribisha msimu mpya


Amesema mchezo huo ni sehemu ya maandalizi ya kikosi chake kuelekea msimu mpya wenye malengo makubwa


"Kesho ni siku kubwa kwa Mashabiki wa Young Africans SC pamoja na sisi wote tunakwenda kupata nafasi ya kusherekea kufunguliwa kwa msimu huu mpya tukiwa na matarajio ya kuendelea kuipambania Klabu hii kubwa yenye historia kubwa"


"Kwenye upande wa timu bado tuko kwenye maandalizi, na mchezo wa kesho dhidi ya Kaizer Chiefs tutautumia kama sehemu ya maandalizi yetu kwa msimu ujao"


"Tunatarajia kuwa na malengo makubwa zaidi kwasababu hii ni klabu kubwa yenye mashabiki wengi wenye nguvu na ushawishi kutaka Klabu hii iendelee kufanya vizuri zaidi hasa kwenye mashindano ya kimataifa," alisema GamondiDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz