Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Gamondi amesema ameifuatilia Yanga iliposhiriki michuano ya CAF msimu uliopita na alifurahishwa na maendeleo na zaidi mipango ya timu
"Nafurahi kujiunga na Yanga, nimeifuatilia Yanga na najua malengo makuu msimu huu ni kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa. Pia nimefurahishwa na mikakati ya timu wakati nilipozungumza na Rais"
"Naamini baada ya kupata mapumziko kutokana na kufanya kazi mfululizo katika nchi mbalimbali, huu ni wakati sahihi kupata changamoto mpya"
"Nipo hapa kufundisha kandanda safi, kuwapa furaha mashabiki na kushinda makombe, naamini tunaweza kufanikiwa malengo yetu," alisema Gamondi
Baada ya Gamondi kutua, wakati wowote Yanga itatangaza benchi lake la ufundi tayari kuanza maandalizi ya msimu mpya (2023/24) ambapo wachezaji wanatarajiwa kuingia kambini Avic Town siku ya Jumatatu
Post a Comment