Yanga kupata gwaride la heshima Mbeya - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga kupata gwaride la heshima Mbeya

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Yanga wako mkoani Mbeya ambapo jioni ya leo saa 10 watashuka uwanja wa Sokoine kumenyana na Mbeya City katika mchezo wa raundi ya 29 ligi kuu ya NBC


Tayari Wananchi wametwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa msimu wa pili mfululizo hivyo leo watakuwa na nafasi ya kupewa gwaride la heshima kutoka kwa Mbeya City


Gwaride kama hilo pia watalipata katika mchezo utakaofuata dhidi ya Tanzania Prisons siku ya Ijumaa, Juni 09 siku ambayo watakabidhiwa taji lao la 29 ligi kuu


Shamrashamra za ubingwa zitaanza Mbeya na kuhitimishwa jijini Dar es salaam Juni 10 kabla ya Yanga kuelekea Tanga wanakokabiliwa na mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Azam Fc


Mkufunzi wa Yanga Nasreddine Nabi leo huenda akawapa mapumziko baadhi ya wachezaji hasa wale waliotumika katika mchezo uliopita wa fainali kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger


Yanga inakabiliwa na ratiba ngumu ya kucheza mechi nne katika siku 9Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz