Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Maboresho ya kikosi cha Simba yanaendelea ambapo mpaka sasa inaelezwa nyota watatu tayari wameshamwaga wino Msimbazi
Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira ambaye yuko mapumziko huko Brazil, ameeleza furaha yake baada ya viongozi wa Simba kukamilisha usajili ambao ni mapendekezo yake
"Hadi sasa tayari kuna wachezaji kama watatu waliokwisha kusajiliwa na wote ni sehemu ya mipango yangu na nimefurahishwa kwa jambo hili, naamini hadi kumalizika kwa orodha niliyoitoa kwenye ripoti yangu nitakuwa na timu bora msimu ujao," Robertinho alinukuliwa na gazeti la Mwanaspoti
"Kazi haijaisha, naamini hadi nitakaporejea kila kitu kitakuwa kimekamilika na kuanza mikakati ya msimu mpya sambamba na michuano ya CAF Super League, ila hadi sasa tupo vizuri kwani naona timu inaenda kubalansi kama anilivyotaka kwa kusainishwa kwa wachezaji hao wa awali"
Kabla hajaondoka nchini kwenda mapumziko Brazili, Robertinho aliwaagiza viongozi wa Simba wahakikishe michakato yote ya usajili iwe imekamilika mwezi huu ili timu itakapoingia kambini mwanzoni mwa mwezi Julai awe na wachezaji wote kwenye pre-season
Nyota ambao wanatajwa kuwa tayari wako mikononi mwa Simba ni pamoja na kiungo mshambuliaji/winga Leandre Onana raia wa Cameroon akitokea klabu ya Rayon Sport
Onana alikuwa mfungaji bora wa Ligi ya Rwanda msimu uliomalizika akiweka kambani mabao 16
Nyota wengine ambao wanatajwa kutua Msimbazi ni Yahya Mbegu kutoka Ihefu Fc na Milton Karisa kutoka klabu ya Vipers Fc ya Uganda ambayo Robertinho alikuwa akiifundisha kabla ya kutua Simba
Aidha Simba tayari imemuongezea mkataba wa miaka mitatu kiungo Sadio Kanoute ambaye mkataba wake ulimalizika mwezi uliopita
Post a Comment