Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Ahmed amesema klabu bado iko kwenye mazungumzo na baadhi ya wachezaji ambao wengine watawasitishia mikataba yao kwa kuwa hawamo katika mipango ya Kocha Robertiho Oliveira katika msimu ujao
"Bado hatujafunga zoezi la kuagana na baadhi ya wachezaji, tuko kwenye mazungumzo ya kusitisha mikataba ya wachezaji ambao hawatakuwa nasi msimu ujao"
"Tunatarajia zoezi hili tutalikamilisha wiki hii ili wiki ijayo tuanze kutambulisha wachezaji tuliowasajili kuchukua nafasi za wachezaji walioachwa," alisema Ahmed
Wachezaji ambao mpaka sasa wamepewa mkono wa kwaheri na klabu ya Simba ni Augustine Okrah, Victor Akpan, Nelson Okwa na Mohammed Ouattara
Wengine ni Beno Kakolanya, Erasto Nyoni na Jonas Mkude
Post a Comment