Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League 2023/2024) umepangwa kuanza rasmi August 09,2023 kwa mchezo wa Fainali ya Ngao ya Jamii kuchezwa katika Uwanja Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.
Imefahamika kuwa Ngao ya Jamii msimu ujao wa 2023/2024 itachezwa kama Mtoano au Nusu Fainali.
Hizi hapa ni timu 4 zitakazoshiriki kuwania Kombe la Ngao ya Jamii, ikiashiria Ufunguzi wa Ligi Kuu ya NBC 2023/2024.
Young Africans
Simba SC
Azam FC
Singida Big Stars
Mfumo utakaotumika kumpata Bingwa na Ratiba kamili tumekuwekea hapa chini;
Nusu Fainali ya Kwanza itakuwa kati ya Simba SC dhidi ya Azam FC tarehe 4 mwezi August 2023 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Nusu Fainali ya Pili itakuwa Kati ya Young Africans dhidi ya Singida Big Stars tarehe 5 mwezi August 2023 kwenye Uwanja wa CCM Sokoine Jijini Mbeya.
Mshindi wa Nusu Fainali ya Kwanza (Simba vs Azam FC) atacheza Fainali dhidi ya Mshindi wa Fainali ya Pili (Yanga vs Singida BS) tarehe 9 mwezi August 2023 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.
Aidha Fainali itachezwa mechi moja tu.
Post a Comment