Mayele, Aziz Ki kuikosa Azam FC fainali ya ASFC Mkwakwani - EDUSPORTSTZ

Latest

Mayele, Aziz Ki kuikosa Azam FC fainali ya ASFC Mkwakwani

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Nyota wawili wa Yanga, Fiston Mayele na Stephane Aziz KI watakosa mchezo wa kesho wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Azam utakaopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.


Mastaa hao ambao wameipatia klabu hiyo ubingwa wa 29 wa Ligi Kuu Bara watakosekana kwenye mchezo huo kutokana na kwenda kwenye majukumu ya timu zao za taifa zinazocheza michezo ya kufuzu AFCON.


Aziz Ki atacheza mchezo huo wa kufuzu AFCON akiwa na Burkina Faso itakayocheza na Cape Verde huku Mayele anayecheza DR Congo atapambana na Gabon ambapo michezo yote hiyo itachezwa Juni 18.


Mbali na kukosa mchezo huo mastaa hao pia watakosekana katika usiku wa tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) zitakazofanyika siku hiyo jijini Tanga baada ya kuisha kwa fainali ya ASFC.


Kutokana na mastaa hao kukosekana kwenye tuzo hizo watachukuliwa hatua za kinidhamu endapo tu watakuwa hawajatoa taarifa kwenye mamlaka husika ikiwemo kupoteza nafasi ya ushindi, kufungiwa na kupigwa faini.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz