Matokeo Mbeya city vs Yanga leo june 6 - EDUSPORTSTZ

Latest

Matokeo Mbeya city vs Yanga leo june 6

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Dakika 45 za kibabe kwenye kipindi cha pili zimeihakikishia Yanga kuondoka na alama moja katika uwanja wa Sokoine baada ya sare ya mabao 3-3 dhidi ya Mbeya City


Salum Abubakar 'Sure Boy' na Bernard Morrison ndio waliohakikishia Yanga alama moja ya kuongezea juu ya alama 74 za ubingwa Yanga ikishuhudiwa ikitoka nyuma kwa mabao 3-0


Sangija na Richardson Ngondya walifunga mabao ya Mbeya City ambayo mpaka dakika ya 64 ilikuwa mbele kwa mabao 3-0 kabla ya Morrison kufunga bao la kwanza la Yanga kwa mkwaju wa penati kwenye dakika ya 65


Sure Boy akaongeza la pili kwenye dakika ya 69 kabla ya Morrison kuisawazishia Yanga kwenye dakika za jiooooni kabisa


Katika mchezo huo winga Jesus Moloko alitolewa nje kwa kadi nyekundu sambamba na Nassor Maulid wa Mbeya City baada ya wachezaji hao kupiganaDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz