Matchday: Tanzania vs Niger leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Matchday: Tanzania vs Niger leo

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo inatupa karata muhimu uwanja wa Benjamin Mkapa ukiwa ni mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya Afcon 2023 dhidi ya Niger


Tanzania inahitaji kushinda leo ili kuweka hai matumaini ya kufuzu huku ikiomba Uganda ipoteze mchezo dhidi ya Algeria ambao utapigwa huko Cameroon


Algeria tayari imefuzu wakati Tanzania, Uganda na Niger bado zinachuana kuwania nafasi ya pili


Tanzania inashika nafasi ya pili kundi F ikiwa na alama nne sawa na Uganda wakati Niger inashika nafasi ya nne ikiwa na alama mbili


Mechi ya mwisho kwa Tanzania ni ugenini dhidi ya Algeria hivyo kufanya mchezo wa leo dhidi ya Niger kuwa lazima kushinda na kwenda kusaka angalau alama moja huko Algeria


Mchezo utapigwa saa 10 jioni katika uwanja wa Benjamin MkapaDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz