Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Paris St-Germain iko tayari kumuuza Kylian Mbappe msimu huu wa joto badala ya hatari ya kumpoteza bila malipo katika muda wa mwaka mmoja, baada ya kuiambia klabu hiyo ya Ufaransa kuwa hataongeza mkataba wake.
Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo wa Ufaransa unamalizika mwishoni mwa msimu ujao, kukiwa na chaguo la kuongeza mwaka mwingine.
Kulikuwa na makataa ya Julai 31 kwa Mbappe, 24, kuiambia PSG kama angepanga kusajili upya mkataba hadi 2025.
Baada ya mazungumzo ya miezi kadhaa, ameitumia klabu hiyo barua akisema hatofanya hivyo.
Mfungaji huyo bora wa PSG atakuwa huru kuondoka bila malipo mwishoni mwa msimu ujao na hatua hiyo inaweza kuwa mbinu ya kufanya mazungumzo.
Hata hivyo, wakati mabingwa hao wa Ufaransa wakijaribu kurekebisha sera ya michezo kwa timu yao baada ya miaka mingi ya kununua wachezaji nyota bila mkakati madhubuti, PSG wameazimia kutomwacha Mbappe kwenda bure, huku klabu hiyo ikikerwa na barua ya mchezaji huyo iliyovujishwa kwenye vyombo vya habari kwanza kabla ya wao kuiona.
Ina maana kwamba wasipopata hakikisho kuhusu nia ya baadaye ya mshindi huyo wa Kombe la Dunia 2018, watamuuza katika hatua ambayo itaweka vilabu vinavyoongoza barani Ulaya kuwa macho.
Real Madrid wanamtamani kwa muda mrefu Mfaransa huyo na alikataa kuhamia Bernabeu kusalia PSG mwaka jana.
Kuondolewa kwa Karim Benzema kwenda Saudi Arabia kunamaanisha kuwa Real inahitaji mshambuliaji, ingawa ilifikiriwa kuwa Harry Kane wa Tottenham alikuwa kileleni mwa orodha yao.
Mbappe, ambaye alijiunga na PSG mwaka 2017 kwa mkopo akitokea Monaco kabla ya uhamisho wa euro 180m na amefunga mabao 212 katika michezo 260.
Ana mabao 38 katika mechi 68 alizoichezea Ufaransa, ikiwa ni pamoja na mabao matatu kwa mpigo katika fainali ya mwaka jana nchini Qatar, Ufaransa iliposhindwa na Argentina kwa mikwaju ya penalti.
Mbappe alimaliza kama mfungaji bora wa Ligue 1 katika kila misimu mitano iliyopita na ameshinda mataji matano ya ligi katika misimu yake sita akiwa PSG.
PSG ilimaliza msimu wa 2022-23 kwa kutwaa taji la Ligue 1 pekee baada ya kushindwa tena kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa, na kufungwa na Bayern Munich katika hatua ya 16 bora.
Mbappe atakuwa mshambuliaji wa pili mwenye hadhi ya juu kuondoka Parc des Princes msimu huu, baada ya mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi kuondoka mwishoni mwa kandarasi yake ya miaka miwili na kujiunga na Inter Miami ya Ligi Kuu ya Soka.
Neymar, mchezaji wa tatu wa safu ya mbele ya nyota wa PSG msimu uliopita, amekuwa akihusishwa na kuhamia Saudi Arabia kwa kitita cha pesa nyingi.
Post a Comment