Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Simba imerejea kwenye harakati za kumsajili winga wa Al Ahly Luis Miquissone ambaye hana nafasi katika kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria ligi ya mabingwa barani Afrika
Miquissone amekuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi sita baada ya muda wa mkopo na klabu ya Abha ya Saudi Arabia kumalizika huku Al Ahly wakimuondoa katika mipango yao
Ni miongoni mwa wachezaji ambao watauzwa na Al Ahly katika dirisha hili la usajili na nafasi kubwa kwake kurejea Simba ni kubwa
Mahusiano mazuri kati ya Simba na Al Ahly yanaweza kurahisisha mazungumzo na pengine Simba kumpata nyota huyo
Hata hivyo, Miquissone atalazimika kupunguza mshahara wake ambapo katika klabu ya Al Ahly anapokea kitita cha Tsh Milioni 95 kwa mwezi
Post a Comment