Hazard atemwa Real Madrid - EDUSPORTSTZ

Latest

Hazard atemwa Real Madrid

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Mchezaji wa Kimtaifa wa Ubelgiji Eden Hazard ameondoka katika klabu yake ya Real Madrid msimu huu wa joto ikiwa imesalia mwaka mmoja kwenye mkataba wake.


Hazard alisajiliwa na Madrid mwaka 2019 kufuatia mafanikio makubwa akiwa Chelsea, lakini sasa ameshindwa kuwa na nyakati nzuri klabuni hapo kutokana na kusumbuliwa na majeraha mengi.


Hazard aling’ara katika Ligi kuu ya Uingereza “English Premier League” na kutimiza ndoto ya kuhamia Madrid, lakini majeraha yameathiri muda wake mwingi akiwa huko.


Taarifa ya klabu ilisema: “Real Madrid CF na Eden Hazard wamefikia makubaliano ambayo mchezaji huyo ataachiliwa huru mnamo Juni 30, 2023.


“Eden Hazard amekuwa sehemu ya klabu yetu kwa misimu minne, ambapo ameshinda mataji 8: Kombe la Uropa x1, Kombe la Dunia la vilabu x1, Kombe la Super Super x1, La Liga x2, Copa del Rey x1 na Super Cups ya Hispania X1.


“Real Madrid inataka kuonyesha mapenzi yake kwa Eden Hazard na inamtakia kila la heri yeye na familia yake katika hatua hii mpya.”Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz